Nahodha wa Lamine Moro hatarajiwi kuwa sehemu ya kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria msimu ujao baada ya kufikiwa makubaliano ya kusitisha mkataba wake, imefahamika
Lamine alikuwa na mkataba wa mwaka mmoja uliokuwa umesalia
Aidha pamoja na Carlinhos na Haruna Niyonzima ambao inafahamika hawatakuwa na Yanga msimu ujao, mshambuliaji Michael Sarpong na kiungo Saido Ntibazonkiza nao mikataba yao inaweza kusitishwa
Saido amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara wakati Sarpong ameshindwa kuonyesha makali yake katika msimu uliomalizika
Mkataba wa Fiston Abdulrazak umemalizika na huenda asipewe mkataba mwingine baada ya kushindwa kuwashawishi Wananchi
Uongozi wa Yanga umedhamiria kukisuka upya kikosi chake kwa kusajili wachezaji watakaokuwa na ushindani zaidi hasa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa