Aliyekuwa nahodha wa Yanga Lamine Moro amewashukuru wanafamilia wa Yanga kwa ushirikiano waliompa katika kipindi cha miaka miwili aliyowatumikia mabingwa hao wa kihistoria
Lamine amesema Yanga ni klabu ya kipekee yenye utamaduni wa kipekee na amefarijika kuwa sehemu ya wachezaji waliopata heshima ya kuitumikia Yanga
"Baada ya miaka miwili kuwa hapa Tanzania, nachukua nafasi hii kusema asante sana kwa Yanga"
"Kwa wafanyakazi wa Yanga, mashabiki na kwa wachezaji wenzangu, pamoja tulipitia nyakati nzuri na mbaya"
"Lakini tulisimama pamoja. Yanga ni klabu ya kupendeza na utamaduni mzuri, siku zote nilihisi niko nyumbani"
"Kwamba ni raha na heshima kuvaa jezi ya Yanga. Nitakumbuka kila wakati tuliokuwa sote Tanzania"
"Nawatakia kila la kheri! Asante Yanga, asanteni sana.."
LAMINE MORO