Tunakwenda kushindana Kagame Cup - Siwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
31 Jul 2021
Tunakwenda kushindana Kagame Cup - Siwa

Kocha Razak Siwa amesema Yanga haiendi kushiriki tu michuano ya kombe la Kagame, bali wamedhamiria kutwaa ubingwa wa michuano hiyo

Yanga itashuka uwanjani kesho Jumapili katika mchezo wake wa kwanza dhidi ya Nyasa Big Bullets utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia saa moja usiku

Siwa amekabidhiwa majukumu ya kuiongoza Yanga katika michuano hiyo inayofanyika Tanzania

Kocha huyo wa makipa katika kikosi cha Yanga, amesema hawafahamu vizuri Nyasa Big Bullets lakini wamejipanga kwa ajili ya kuwakabili na kuhakikisha wanashinda mchezo wao wa ufunguzi wa michuano hiyo

"Sina takwimu zao vizuri, lakini cha msingi ni kuingia kwenye michuano kwa malengo. Na sisi lengo la ushiriki ni kutwaa ubingwa, hivyo tuna kila sababu ya kuingia kwa tahadhari zote ili tupate ushindi," alisema Siwa

Kikosi cha Yanga kiliingia kambini jana kujiandaa na michuano hiyo, kikiundwa na wachezaji wazoefu na wale wa kikosi cha vijana

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
48m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
21h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’