FT : Yanga 2-1 Mlandege FC

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Jan 2018
FT : Yanga 2-1 Mlandege FC
Yanga imeanza vyema mashindano ya kombe la Mapinduzi baada ya kuilaza timu ya Mlandege mabao 2-1 katika mchezo mkali uliopigwa kwenye dimba la Amani Jumanne usiku.

mabao yote ya Yanga yalifungwa na mshambuliaji Juma Mahadhi ambaye mapema leo aliweka wazi mipango yake mwaka huu 2018 akiomba mashabiki na benchi la ufundi limwamini.

Imani aliyopewa leo na kocha Shedrack Nsajigwa na mwenzie Noel Mwandila imezaa matunda na huenda imefungua ukurasa mpya kwa mshambuliaji huyo mwenye kipaji cha hali ya juu.

Mabao yote yalitengenezwa na walinzi wa pembeni Hassani Kessy na Mwinyi Haji.

Mlandege iliyotoa upinzani mkali kwa Yanga ilijipatia bao pekee kupitia kwa Omary Makame aliyepiga shuti kali nje kidogo ya 18 baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa Yanga.

Katika dakika ya kwanza ya mchezo Yanga ilipata pigo pale beki wake Abdallah Sahibu 'Ninja' alipotolewa nje baada ya kugongana na mshambuliaji wa Mlandege kupelekea akapoteza fahamu.

Beki huyo anayekuja kasi anaendelea vizuri, nafasi yake ilichukuliwa na nahodha Nadir Haroub 'Cannavaro'.

Yanga ikapata pigo tena wakati mchezo huo unaelekea ukingoni baada ya beki kisiki Andrew Vicent 'Dante' kutolewa nje kwa kadi nyekundu sambamba na mshambuliaji wa Mlandege Ali Makame baada ya kutokea sintofahamu baina yao.

Makame alijiangusha ndani ya eneo la hatari akijaribu kumdanganya mwamuzi ili apate penati tukio lililomkera Dante.

Ushindi huo unaweka hai matumaini ya Yanga kufanya vizuri kwenye michuano hiyo.

Aidha ni jambo jema kwa benchi la ufundi kutumia michuano hii kuwapa nafasi wachezaji wasiotumika sana katika kikosi cha kwanza.

Wataweza kupata uzoefu na kuongeza kujiamini hivyo kuwa tayari kutumika kwenye ligi.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
7h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
23h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’