Aliyekuwa Msemaji wa Simba Haji Manara amewaomba radhi Yanga kutokana na kauli aliazokuwa akitoa wakati akiwa kiongozi wa Simba
Manara amesema anafahamu alikuwa akiwakwaza wengi wakiwemo wanahabari hivyo anamba radhi
"Nawaomba radhi Yanga, Wanahabari. Kuna wakati nilivuka mipaka na kuzungumza maneno yasiyo ya kiungwana hivyo naomba mnisamehe," alisema Manara
Aidha Manara amefichua kuwa klabu ya Simba ilisaini mkataba wa maudhui na Azam Media wenye thamani ya Tsh Milioni 385 kwa mwaka lakini baadae viongozi wa timu hiyo waliwasiliana na viongozi wa Yanga wakiomba kwenda kuanzisha majadiliano ya pamoja ya mkataba na Azam Media
Manara ameeleza kushangazwa na kauli iliyotolewa na Mwekezaji wa Simba Mohammed Dewji 'Mo' kuwa hawako tayari kusaini mkataba wenye maslahi sawa na Yanga kwa kuwa klabu yao ni kubwa
"Kama mnajua Simba ni kubwa, kwanini mliwafuata Yanga Sc mkaenda nao Azam Media kujadili dili la maudhui? Kama Simba ingekuwa kubwa kiasi hiko si wangeenda wenyewe tu Azam Media kwanini hamukuwaita Ihefu?," alihoji Manara