Mshambuliaji mpya wa Yanga Heritier Makambo leo ametembelea kambi ya kikosi cha Yanga kinachojiandaa na mchezo wa tatu kombe la Kagame dhidi ya Express Fc
Makambo sio miongoni mwa wachezaji walioandikishwa kushiriki michuano hiyo iliyoanza August 01, lakini yuko nchini akisubiri kuanza rasmi maandalizi ya msimu mpya baada ya kumalizika michuano ya Kagame
Ilikuwa faraja kwa baadhi ya wachezaji kuonana ana kwa ana na Makambo ambapo wachezaji kama Paulo Godfrey 'Boxer', Abdallah Shaibu 'Ninja', Ramadhani Kabwili alikuwa nao katika kikosi mwaka juzi


ADVERTISE HERE