Hatua ya makundi michuano ya kombe la Kagame inafikia tamati kesho Jumamosi ambapo Yanga itashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Express katika mchezo utakaopigwa kuanzia saa kumi Alasiri
Yanga inahitaji matokeo ya ushindi dhidi ya vinara hao wa kundi A kujihakikishia kutinga nusu fainali
Yanga imeshindwa kupata ushindi katika michezo miwili iliyopita wakilazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Nyasa Big Bullets na suluhu ya bila kufungana dhidi ya Atlabara Fc
Ni matokeo yaliyowavunja moyo mashabiki wa Yanga ambao walikuwa na matumaini makubwa kwa timu yao kufanya vizuri katika michuano hiyo
Kukosekana kwa uzoefu kwa baadhi ya wachezaji wanaotumika katika michuano hiyo inaweza kuwa moja ya sababu iliyopelekea Yanga kutotamba
Yanga imetumia michuano ya Kagame kuwapa nafasi baadhi ya wachezaji ambao hawakutumika sana kwenye kikosi cha kwanza, wachezaji wa kikosi cha vijana na baadhi ya nyota wapya waliosajiliwa
Hata hivyo, Yanga imeonekana kuimarika mchezo hadi mchezo, nafasi ya kushinda mechi dhidi ya Express ni kubwa