Winga mshambuliaji wa Yanga Juma Mahadhi Juma Mahadhi ametoa shukrani kwa benchi la ufundi kwa kumuamini na kumpa nafasi kwenye mchezo wa jana dhidi ya Mlandege.
Katika mchezo huo ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 Mahadhi alifunga mabao yote ya Yanga.
Akizungumza baada ya mchezo, Mahadhi amesema mwaka huu 2018 amedhamiria kurejesha makali yake aliyokuwa nayo wakati anasajiliwa na Yanga akitokea Coastal Union miaka miwili iliyopita.
Amesema ametambua makosa yake na atahakikisha hayarudii na kikubwa amefurahi kwa kuanza mwaka na mwanzo mzuri.
"Nimekuwa nikilaumiwa sana na mashabiki na hata viongozi wangu kuwa kiwango changu hakiko sawa, nahitaji kujituma zaidi."
"Wengi waliamini mimi ndiye ningeweza kuziba pengo la Simon Msuva, nilikuwa naumia sana," alisema Mahadhi.
"Lakini nawaahidi mwaka huu nitakuwa tofauti sana, nitahakikisha naisaidia timu yangu ipasavyo kila nitakapopewa nafasi"
Mahadhi ameanza kwa kubadilisha mwonekano wake ambapo ameondoa rasta zake na kunyoa kawaida.
Mashabiki wengi walikuwa wakimkosoa kuwa anatumia muda mwingi kwenye kutunza nywele zake kuliko kuboresha kiwango chake.

ADVERTISE HERE