Yanga imetambulisha usajili wa Djgui Diarra mlinda lango wa Kimataifa kutoka Mali
Diarra ametua kuchukua nafasi ya Farouk Shikhalo aliyemaliza mkataba na Wananchi
Michuano ya Kagame ilikuwa na mwisho kwa Shikhalo aliyejiunga na Yanga miaka miwili iliyopita
Diarra anakwenda kuwa kipa namba moja wa Yanga huku tetesi zikibainisha kuwa atasaidiwa na Erick Johora aliyesajiliwa kutoka klabu ya Aigle Noir huku Ramadhani Kabwili akitarajiwa kuendelea kuwa mlinda lango namba 3
Yanga imedhamiria kumaliza changamoto ya golikipa iliyowatesa Wananchi msimu uliopita
ADVERTISE HERE