Uongozi wa klabu ya Yanga umetangaza kuachana na waliokuwa walinda lango wake Metacha Mnata na Farouk Shikhalo
Akizungumza na Azam Media wakati wa utambulisho wa kiungo mpya Khalid Aucho, Kaimu Katibu Mkuu Haji Mfikirwa amesema uongozi wa Yanga unawashukuru magolikipa hao kwa miaka miwili waliyoitumikia Yanga
Amesema tayari wamekabidhiwa nyaraka muhimu kuwatambulisha kuwa ni wachezaji huru
Aidha kuhusu Tuisila Kisinda, Mfikirwa amethibitisha ni kweli ameuzwa nchini Morocco
ADVERTISE HERE