Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Haji Mfikirwa amethibitisha kuwa klabu hiyo imemuuza winga Tuisila Kisinda kwenda klabu ya RS Berkane ya Morocco
Mfikirwa amesema dau la usajili wa mchezaji huyo ni dola 150,000 ambazo ni karibu Mil 350 fedha za Kitanzania
Aidha, Mfikirwa amesema pamoja na dau hilo, Yanga imepata ofa ya kufanya pre-season nchini Morocco
Mfikirwa amesema RS Berkane wametoa ofa nzuri zaidi ya mshahara kwa Kisinda na pia kwa upande wa Yanga, yeye akiwa Mhasibu hakuona shida kuidhinisha
Amesema wataleta mchezaji mwingine kuchukua nafasi ya Kisinda
Kisinda alikuwa amesalia na mkataba wa mwaka na Yanga
Ameenda kuungana na kocha wake wa zamani katika klabu ya AS Vita Florente Ibenge
ADVERTISE HERE