Jana beki Kelvin Yondani na Ibrahim Ajib walikuwa miongoni mwa wachezaji waliofanya mazoezi kwenye uwanja wa Bumbwi Sudi, kisiwani Zanzibar kujiandaa na mchezo wa pili wa kombe la Mapinduzi dhidi ya JKU leo.
Yondani amekuwa nje kw atakribani mwezi mmoja tangu aumie kwenye michuano ya kombe la Chalenji nchini Kenya wakati akiitumikia Kilimanjaro Stars mwezi Disemba mwaka jana.
Kurejea kwake dimbani ni habari njema kwa kikosi cha Yanga kitakachomkosa beki Andrew Vicent 'Dante' aliyeonyeshwa kadi nyekundu katika mchezo uliopita.
Aidha Abdallah Shaibu 'Ninja' naye aliumia katika mchezo huo dhidi ya Mlandege na huenda asiwe tayari kushuka dimbani leo licha ya kurejea mazoezini.

ADVERTISE HERE