Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi Dominic Albinus ametoa maoni yake kufuatia sintofahamu iliyojitokeza baada ya ofa ya Tuisila Kisinda kutoka RS Barkane
Albinus amesema kwa kitendo cha timu nyingine kuleta ofa kuwataka wachezaji wa Yanga ni jambo la kujivunia kuwa klabu inafuatiliwa huko nje
Lakini amefafanua, pamoja na kupokea ofa kwa ajili ya wachezaji wengine pia, hawafikirii kuuza mchezaji mwingine kwani wanafahamu wakifanya hivyo wataathiri uimara wa timu
Ujumbe wake huu hapa
Yanga inapata offers nyingi kwa wachezaji wao,Wanayanga hawajivunii wanawasakama viongozi wao na kuingiwa Ubaridi
Kwangu nadhani ishu ya kwanza ni Wanayanga kujivunia kuwa na wachezaji wenye ubora unaotambulika na kuheshimika Nje ya Mipaka ya Afrika
Biashara ya Mpira haiepukiki. Ukiwa timu inayofuatiliwa ndivyo unavyojipambanua kuwa daraja la juu. Unapokuwa klabu ambayo wachezaji bora wanakiri kushawishika kujiunga nawe , inakudhihirishia daraja lako kuwa ni kubwa kiasi gani
Platform ya Yanga Sc kupitia Tuisila Kisinda Deal to RS Berkane iliyoko Morocco inakuonyesha Yanga Sc inafuatiliwa kwa ukubwa gani.
Sajili za Yanga msimu huu kwa wachezaji wakubwa toka mataifa kama ya Congo, Mali, Burkina Faso na Uganda inadhihirisha ukubwa wa Ushawishi wa Klabu hii na Ligi ya Tanzania kwa Ujumla
Hii imetokea kwa vilabu vyote vikubwa vikubwa vitatu katika ushawishi wa kusajili Top Class na Top performers wao kuhitajika katika vilabu vikubwa Afrika.
Kama nilimuelewa vyema Eng. Hersi,hakusema klabu itawauza akina Mukoko na Yacouba Sogne kama inavyoonekana kwa Tuisila Kisinda
Alidhihirisha ya kwanza kuna Ofa kadha wa kadha kwa wachezaji wao bora na wao kama klabu wanazifanyia tathmini kwa malengo makubwa ya klabu ya Yanga .
Hivyo , Si kweli kuwa Yanga Sc itawauza wachezaji hawa wote. Pia haiwezi ingia akilini Kuuza wachezaji wako bora wa 3 kwa mpigo ilhali wewe pia ni katika timu inayojijenga kuwa stable kiushindani katika mashindano ya ndani na kimataifa
Kiufundi hii haiwezi kukupa balance sahihi katika process ya kuimarisha kikosi na ujenzi wa Kikosi bora cha Ushindani. . Mpira umekuwa biashara kubwa Duniani, Afrika na Tanzania, Japokuwa mwamko wa Mtazamo huu kwa nchi yetu umeanza kudhihirika kipindi hiki.
Players, Coaches come And Go. . But Top Clubs always works to bring about the best out the situations kwa maslahi mapana ya klabu ya muda mfupi na mrefu. .
Naamini , Best players wanaweza Uzwa kwa faida , Crucial Top players wataongezewa mikataba kulinda Misingi ya Ubora wa kikosi.