Uongozi wa Yanga umethibitisha kuwa wataelekea nchini Morocco kuweka kambi ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi na michuano ya Kimataifa
Wachezaji wa Yanga wameanza kurejea jijini Dar es salaam wakitoka mapumziko tayari kwa safari hiyo
Wakati Yanga wakijipanga na safari, watani zao Simba wanaondoka leo kuelekea huko Morocco ambako nao wanaweka kambi
Hii ni mara ya kwanza kwa timu hizo kuweka kambi nje ya Tanzania pamoja katika nchi moja
Yanga na Simba zitafungua msimu mpya kwa mchezo wa Ngao ya Jamii utakaopigwa Septemba 25 2021
Aidha timu hizo pia zinakabiliwa na mechi za hatua ya awali michuano ya ligi ya mabingwa zitakazopigwa mwanzoni mwa Septemba
ADVERTISE HERE