Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Yanga Dominic Albinus 'Baba Paroko' amesema mlinzi Shabani Djuma atawasili nchini kabla ya August 13 tayari kwa maandalizi ya safari ya Morocco ambako Yanga inakwenda kuweka kambi
Albinus amesema Djuma na wachezaji wengine wataingia kambini Avic Town, Kigamboni kwa ajili ya kukamilisha maandalizi ya mwisho ya safari hiyo itakayokuwa Jumapili, August 15
Kumekuwa na maneno mengi huko mitandao kuhusu Djuma zikizushwa tetesi kuwa mchezaji huyo ametimkia RS Berkane kuungana na aliyekuwa kocha wake AS Vita, Florente Ibenge ambaye pia tayari amemsajili Tuisila Kisinda
Uzushi huo ulishika kasi baada ya kuona Djuma hakuja nchini kutambulishwa kama ilivyo kwa wachezaji wengine waliosajiliwa
Hata hivyo imeelezwa kuwa Djuma hakulazimika kuja nchini kwa kuwa usajili wake ulikamilishwa DR Congo

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano Injinia Hersi Said alikwenda DR Congo kumalizana na Djuma akisaini mkataba wake huko
Wachezaji waliokuja nchini wao hawakupelekewa mikataba katika nchi zao, hivyo walikuja kwa ajili ya kusaini mikataba na hata baada ya zoezi hilo kukamilika waliruhusiwa kurejea makwao