Shirikisho la soka Afrika (CAF) linatarajiwa kutangaza draw ya michezo ya awali (Preliminary) ya CAF Champion League na CAF Confederation Cup Ijumaa August 13 Cairo, Misri
Tanzania ni miongoni mwa mataifa 12 ambayo yatawakilishwa na timu nne ikiwa timu mbili kwenye mashindano ya CAF Champion League na timu mbili kwenye mashindano ya CAF Confederation Cup
Kwa mujibu wa kalenda ya CAF hatua ya awali (Preliminary) kwa michezo ya mkondo wa kwanza itachezwa September 10-12 huku michezo ya marudiano kwa hatua ya awali (Preliminary) itachezwa September 17-19
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) lilikutana na klabu za Tanzania zitazoshiriki michuano hiyo Simba, Yanga, Azam Fc na Biashara United
ADVERTISE HERE