Yanga imeachana na mpango wa kumsajili kiungo mshambuliaji Jimmy Ukonde Julio raia wa Msumbiji
Ukonde alikuwemo katika kikosi cha Yanga kilichoshiriki michuano ya kombe la Kagame
Nyota huyo hakuwa amesajili, benchi la ufundi chini ya kocha Nasreddine Nabi walihitaji kumtizama kabla ya kuidhinisha usajili wake
Hata hivyo nyota huyo anayetumia mguu wa kushoto ameshindwa kumshawishi Nabi
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema wanakamilisha usajili kwa kutambulisha nyota wawili wa kigeni, Ukonde sio miongoni mwao
ADVERTISE HERE