Yanga inatarajiwa kuondoka jijini Dar es salaam wakati wowote kuelekea Morocco kuweka kambi ya maandalizi ya msimu mpya
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema watakwenda Morocco wakiwa na kikosi cha wachezaji 28 ambao wamesajiliwa kwa ajili ya michuano mbalimbali ya msimu ujao
Kikosi kinachotarajiwa kitakuwa na nyota hawa;
Golikipa: Diarra Djigui, Erick Johora na Ramadhan Kabwili
Walinzi: Bakari Mwamnyeto, Abdallah Shaibu, Dickson Job, Kibwana Shomari, Yassin Mustapha, Adeyum Saleh, Paul Godfrey, David Bryson, Djuma Shaban na Yannick Bangala
Viungo: Deus Kaseke, Feisal Salum, Zawadi Mauya, Mapinduzi Balama, Mukoko Tonombe na Khalid Aucho
Washambuliaji: Farid Mussa, Ditram Nchimbi, Yacouba Sogne, Saido Ntibazonkiza, Yusuf Athuman, Dickson Ambundo, Fiston Mayele, Heritier Makambo na Jesus Moloko
Msafara huo pia utawajumuiisha viongozi 9 wa benchi la ufundi chini ya kocha mkuu Nesreddin Nabi na wasaidizi wake, Shir Hammadi, Jawad Sabri na Razack Siwa, meneja Hafidh Saleh, watunza vifaa Mahmoud Omary, Mohamed Mposo, Daktari Shecky Mngazija, Mtaalam wa misuli Jacob Onyango na viongozi sita wa klabu
Kambi itakuwa ya siku zisizozidi 11 wakiweka kambi katika Akademi ya soka ya Mohammed VI ambapo ndani kuna majengo makubwa ya kiutawala, hospitali, viwanja vinne vya mazoezi vya kisasa vya nyasi bandia na nyasi asilia vyenye ukubwa tofauti
Kuna mabwawa ya kisasa, kumbi za chakula na mikutano pamoja na vyumba vya malazi vyenye hadhi ya hoteli ya nyota tano
Viwanja vyote vinne kila kimoja kina urefu wa Mita 105 na upana wa Mita 68 lakini kuna kingine kidogo cha mraba ambacho kina urefu wa mita 48.