Wachezaji wa Yanga leo wanaingia kambini Avic Town, Kigamboni kukamilisha maandalizi ya safari ya Morocco
Yanga itaondoka jijini Dar es salaam keshokutwa Jumapili kwenda Morocco kuweka kambi ya siku 11
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema wachezaji wote wa ndani na baadhi ya nyota wa kigeni, wanaingia kambini Kigamboni leo
Wachezaji wengine wa kigeni waliosajiliwa karibuni na kuruhusiwa kurejea makwao, wataungana na timu Morocco
Aidha Bumbuli amethitisha kuwasili wa wachezaji Shabani Djuma na Jesus Moloko waliotua Alfajiri ya leo
Wachezaji hao watatambulishwa wakati wowote huku akibainisha kuwa kutakuwa na utambulisho wa mchezaji mwingine raia wa kigeni ambaye naye yuko njiani (Yannick Bangala Litombo)
ADVERTISE HERE