Dirisha la usajili kwa ajili ya michuano ya ligi ya mabingwa linafungwa kesho Jumapili, saa 5.59 usiku Yanga ikitarajiwa kukamilisha michakat yake leo
Wananchi wanatarajiwa kukamilisha hesabu zao kwa utambulisho wa mlinzi wa kati, Yannick Bangala anayekuja kuchukua nafasi ya Lamine Moro
Aidha taarifa za ndani, zimedokeza kuwa kunaweza kuwa na usajili mwingine wa 'sapraizi' katika dakika za majeruhi
Idadi kubwa ya wachezaji waliosajiliwa kwa ajili ya msimu ujao tayari wako kambini Avic Town, leo walikikamilisha taratibu za safari ya Morocco
Leo kutakuwa na zoezi la kupatiwa chanjo ya corona kwa wachezaji ambao hawakuwa wamepata chanjo hiyo
Yanga inaondoka jijini Dar es salaam kesho Jumapili kuelekea Morocco
ADVERTISE HERE