Winga Farid Mussa ni miongoni mwa wachezaji wanaotarajiwa kuondoka na kikosi cha Yanga kuelekea Morocco kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi na Michuano ya CAF
Farid ameongeza mkataba wake na klabu ya Yanga baada ya ule wa mwaka mmoja aliosaini awali kumalizika
Farid ni nyota mwenye kipaji kikubwa ambacho bado Wananchi hawajakifaidi
Baada ya kucheza nchini Hispania kwa miaka minne, Farid alirejea na kuitumikia Yanga msimu uliopita
Hakuwa katika ubora ambao wengi wanatamani kumuona lakini ana nafasi nyingine ya kudhihirisha msimu ujao
Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi ameonyesha kuwa na imani nae, bila shaka atakuwa na wakati mzuri
ADVERTISE HERE