Kiungo wa Yanga Mukoko Tonombe 'Teacher' ni miongoni mwa wachezaji walioitwa katika kikosi cha timu ya Taifa DR Congo kinachojiandaa kucheza na timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia nchini Qatar 2022
DR Congo itacheza na Stars, Septemba 3 mchezo utakaopigwa nchini Congo
Mukoko amejumuishwa katika kikosi hicho chenye wachezaji 24 kwa mara ya tatu tangu alipojiunga na Yanga
Wachezaji wengine wanaounda kikosi cha DR Congo ni makipa, Joel Kiassumbua, Herve Lomboto na Bagio Siadi
Mabeki ni Joel Ikoko, Mukoko Amale, Christian Luyindama, Chris Mavingq, Chancel Mbemba,Marcel Tisserand, Glody Ngonda na Fabrice Nsakala
Viungo Edson Kayembe, Mukoko Tonombe, Fabrice Ngoma, Gael Kakuta, Samuel Moutousamy na Neeskens Kabano.
Wakati eneo la ushambuliaji likiwa na Chadrack Akolo, Brit Assombalonga, Cedric Bakambu, Yannick Bolasie, Meshack Elia, Jackson Muleka na Dieumerci Mbokani.