Siwa afurahia kambi Morocco

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Aug 2021
Siwa afurahia kambi Morocco

Mkufunzi wa makipa Yanga Razak Siwa ameeleza kufurahishwa na kambi ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu na michuano ya Kimataifa kupelekwa nchini Morocco

Siwa aliondoka na kikosi jana akiongoza benchi la ufundi ambapo Kocha Mkuu Nasreddine Nabi na Wasaidizi wake wataungana nao nchini Morocco

Siwa amesema walihitaji kambi itakayokuwa na utulivu ili kuweza kuwaunganisha wachezaji wapya na wale wanaoendelea nao

Amesema kambi hiyo itawasaidia kukiimarisha kikosi chao kabla ya kuanza kwa mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Rivers United ya Nigeria

Siwa ameeleza kuona wachezaji wote wapo kwahiyo maandalizi yao yatafanyika kikamilifu lengo kubwa ni kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye michuano yote.

Kwaupande wake Meneja wa timu hiyo, Hafidh Salehe, alisema kambi hiyo inatoa nafasi nzuri kwa benchi la ufundi na wachezaji kujipanga vizuri kabla ya msimu mpya kuanza

"Hongera kwa uongozi wetu kufanikisha kambi, hii ambayo itawasaidia wachezaji na sisi benchi la ufundi kujiandaa na kuweka malengo yetu sawa katika. msimu mpya tunaoelekea kuuanza mwezi ujao, wachezaji wote wapya na wazamani wote tupo safarini," alisema Hafidh

Yanga imeondka nchini na kikosi cha wachezaji 28 na viongozi 16 wa benchi la ufundi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
5h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
9h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
14h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’