Kikosi cha Yanga kimewasili Morocco katika jiji la Casablanca tayari kuanza maandalizi ya msimu mpya wa ligi na michuano ya Kimataifa.
Yanga iliondoka jijini Dar es salaam jana kuelekea Morocco wakipitia DubaiΒ
Wamewasili Morocco majira ya mchana wa leo wakiwa na kundi la wachezaji 21
Wachezaji hao, wameungana na wenzao watatu mlinda lango Diarra Djigui, beki Yannick Bangala na mshambuliaji Yacouba Sogne ambao walishawasili nchini humo
Aidha, kiungo Khalid Aucho anatarajiwa kuwasili Morocco siku ya kesho Jumanne
Kocha Mkuu Nesreddine Nabi na wasaidizi wake wawili nao walishawasili Morocco tayari kuanza maandalizi hayo
Yanga itakuwa na takribani siku 11 za maandalizi kabla ya kurejea Tanzania kwa ajili ya kilele cha Wiki ya Mwananchi August 29 2021