Yanga ilipeleka mashitaka Mahakama ya Kimataifa ya usuluhishi wa michezo (CAS) wakipinga kile walichofanya Simba katika kumsajili Bernard Morrison na baadae kuhalalishwa na Kamati ya TFF
Hukumu ya kesi hiyo itatolewa na CAS kabla ya August 24 2021
Ujanja ujanja kama huo ulitaka kufanywa tena katika usajili wa Yusufu Mhilu ambaye hivi karibuni alitambulishwa na Simba wakati akiwa na mkataba na Kagera Sugar
Kulingana na mchambuzi mahiri wa michezo Ali Kamwe, Kagera Sugar hawajatoa 'Release Letter' kwa Mhilu kusajiliwa na Simba kwa ajili ya michuano ya ligi ya mabingwa. Hivyo Mhilu anaweza asiwe sehemu ya kikosi cha Simba kitakachocheza michuano hiyo
Inadaiwa kuwa katika mazungumzo ya awali, Simba waliwasiliana na uongozi wa Kagera Sugar, wakawasilisha ofa ya Mil 35 lakini Kagera wakaipiga chini wakitaka Mil 50 ili wamtoa Mhilu
Wakati mazungumzo hayo yakiendelea, Simba wakamtambulisha Mhilu, kitendo kilichowakwaza viongozi wa Kagera wakihisi 'kudharauliwa'
Baadae mmoja wa viongozi wa Simba aliwaomba radhi Kagera kuwa utambulisho ule ulifanywa kimakosa na mtu mmoja wa Idara ya Habari, hivyo wakawaomba wasikanushe chochote huku mazungumzo yakiendelea
Lakini Kagera wakashtuka baada ya kuitwa TFF kuwa wamefunguliwa mashitaka na Mhilu akitaka kuvunja mkataba na baada ya kesi kusikilizwa na Kagera kuonekana wana haki na Mhilu anatakiwa kufata Taratibu vizuri za klabu ili kuvunja mkataba
Uongozi wa Kagera sasa umepanga kuishitaki Simba kwa kumtambulisha mchezaji wao na kuhitaji kiasi cha TSH MIL 200 ili wamruhusu
Tukio hili linafanana kabisa na lile sakata la Morrison ambaye nae aliishitaki Yanga akidai kuwa hana mkataba nayo
Wakati kesi ikiendelea Simba wakamtambulisha Morrison kuwa mchezaji wao halali