Ahadi ya Makambo ni mwendo wa 'kuwajaza' tu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Aug 2021
Ahadi ya Makambo ni mwendo wa 'kuwajaza' tu

Mshambuliaji Heritier Makambo ameeleza furaha yake baada ya kurejea Yanga huku akikiri kuwa Yanga ya sasa sio ile aliyotumikia miaka miwili iliyopita

Makambo aliitumikia Yanga kwa mara ya kwanza msimu wa 2018/19 akifunga mabao 22 katika mashindano yote

Mshambuliaji huyo aliyerejea akitokea klabu ya Horoya Ac, ni miongoni mwa wachezaji ambao wako kambini Morocco katika pre-season

"Namshukuru Mungu kwa kupata nafasi nyingine ya kuwa ndani ya Yanga, nawaambia mashabiki wasubiri kuona makubwa kwani tutapambana sana. Nimerejea nimekuta mambo mengi yamebadilika, ninajitahidi kuzoea mazingira haraka, binafsi najivunia kuwa hapa," alisema Makambo

Aidha, Makambo amesema anatarajia ushindani wa namba utakuwa mkubwa kikosini kutokana na usajili uliofanyika

"Ushindani utakuwa mkubwa sana msimu ujao, ukiangalia kila mchezaji ni mzuri, nitajitahidi sana kupambana kupata nafasi ndani ya kikosi cha kwanza, na kupitia pre-season nahisi nitaweza kujiweka sawa kufanya vizuri"

Makambo amesema hii itakuwa nafasi yake ya kwanza kuitumikia Yanga kwenye michuano ya ligi ya mabingwa na mkakati walionao wachezaji ni kuona wanafika mbali katika michuano hiyo

"Ndani ya Yanga hii ni mara ya kwanza nashiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa, lakini nikiwa timu nyingine nimewahi kushiriki. Kutokana na uzoefu wangu, hakuna mashindano mepesi, lazima tutakutana na ugumu, lakini itategemea na maandalizi ya timu"

"Tutajiandaa vizuri. Yanga ni timu kubwa na kutokana na pre-season hii ilivyo nzuri na usajili uliofanywa, ninaimani tutafika mbali sana," aliongeza Makambo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’