Nabi arudi na msimamo uleule katika nidhamu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Aug 2021
Nabi arudi na msimamo uleule katika nidhamu

Msimu uliopita kuna wachezaji waliingia matatani mbele ya kocha Nasreddine Nabi kutokana na matukio ya utovu wa Nidhamu

Lamine Moro, Michael Sarpong, Metacha Mnata na Fiston Abdulrazak ni miongoni mwa wachezaji ambao walionja 'joto ya jiwe' kwa kuzuiwa kufanya mazoezi na hata kusimamishwa kutokana na kutohudhuria au kuchelewa mazoezini

Nyota hao wote hawako kwenye kikosi cha Yanga kinachoendelea na pre-season nchini Morocco

Nabi ameendelea kuweka msisitizo katika nidhamu ambapo amewaambia wachezaji wake hataangalia jina la mchezaji, wote wanapaswa kufuata kile wanachoelekezwa

Nabi amesema ili Yanga ifikie malengo yake wachezaji na watu wake kwenye benchi la ufundi wanatakiwa kuheshimu muda kwa kila eneo kufika kwa wakati bila kuchelewa

Wakati huu amekuja na utaratibu mpya ambapo kama mchezaji atashindwa kuheshimu muda adhabu ya kwanza atakatwa dola 100 (Sh 230,000) kwa kila hatua ya kuchelewa

"Tunatakiwa kufanya mambo yetu kwa kuheshimu muda hii ndio hatua ya kwanza ya nidhamu yetu,ukiwa na nidhamu ya kuheshimu muda hata uwanjani utakuwa makini na na ndio maana nimewaambia sasa," Nabi alinukuliwa na Mwanaspoti

"Hii sio kwa wachezaji tu hata sisi watu wa benchi la ufundi nimewaambia kama kuna mtu atafanya makosa atakumbana na dhabu na hili nitasimamia mimi mwenyewe ili mambo yaende kwa haraka."

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
58m ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
9h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’