Yanga inaendelea na pre-season Morocco kujiandaa na msimu mpya wa ligi na michuano ya Ligi ya Mabingwa
Leo Wananchi wanaingia siku ya nne tangu walipotua Morocco mwanzoni mwa wiki hii
Mapema tu, kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi anafurahia kufanya kazi na wachezaji wapya waliosajiliwa katika dirisha hili la usajili

Aidha Nabi ameonekana kuvutiwa na washambuliaji Heriter Makambo na Fiston Mayele ambao wanafanya vizuri mazoezini
Makambo na Mayele wamezikamata haraka mbinu za Nabi wakifunga mabao mengi mazoezini
Nyota hao wametua kuchukua nafasi zilizoachwa na Fiston Abdulrazak na Michael Sarpong
Wanaunda safu ya ushambuliaji hatari wakiungana na Yacouba Songne pale mbele
Makambo amesema amerejea kuwapa furaha mashabiki wa Yanga akilikumbuka lile jina la Makambovic alilopewa na Baraka Mpenja , mtangazaji wa Azam Tv