Mlinzi wa Kimataifa wa DR Congo Yannick Bangala aliyesajiliwa na Yanga, amesema malengo ya timu na usajili vimemshawishi kujiunga na mabingwa hao wa kihistoria
Bangala amefichua kuwa kabla ya kusaini mkataba wa kuitumikia Yanga, alipata nafasi ya kuzungumza na kocha Nasreddine Nabi ambapo alimueleza malengo ya timu msimu ujao
"Nimejiunga na Yanga baada ya kushawishika na mipango ya timu pamoja na usajili uliofanyika. Nilipata nafasi ya kuzungumza na kocha ambapo aliniambia mipango mikubwa ya Yanga kufanya vizuri katika soka la Afrika na ligi ya Tanzania"
"Nimevutiwa na usajili uliofanyika pia nami kuona naweza kuongeza nguvu katika ushiriki wa timu kwenye mashindano mbalimbali ikiwa ni pamoja na ligi ya mabingwa," alisema Bangala
Bangala ametua Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea klabu ya FAR Rabat iliyomaliza katika nafasi ya tatu ligi kuu ya Morocco
Ameungana na wachezaji Shabani Djuma, Fiston Mayele, Mukoko Tonombe na Jesus Moloko aliowahi kuwa nao kunako klabu ya AS Vita