Wiki ya Mwananchi itakuwa ya kipekee

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
21 Aug 2021
Wiki ya Mwananchi itakuwa ya kipekee

Kuelekea kilele cha Wiki ya Wananchi, uongozi wa Yanga umepanga kuweka rekodi mpya tofauti na ilivyokuwa katika msimu uliopita 

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa, Suma Mwaitenda alisema kumalizika kwa msimu uliopita ni mwanzo wa msimu mpya ambapo katika kilele cha sherehe hizo, wanatarajia kufanya shughuli mbalimbali za kijamii pamoja na uzinduzi wa jezi mpya.

Mwaitenda alisema kilele cha Wiki ya Wananchi kitakuwa ni Agosti 29, mwaka huu wakati uzinduzi utafanyika kesho Jumapili huko Zanzibar na mgeni rasmi ni Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hemed Suleiman.

"Lengo la Wiki ya Wananchi ni kurudisha shukrani zetu kwa mashabiki kwa kufanya mambo mbalimbali ikiwamo kuchangia damu, kupanda miti na kutoa msaada kwa wasiojiweza, tutafungua matawi mawili pamoja na kugawa magodoro katika Hospitali mbili za Mwembeladu na Mnazi Mmoja," alisema Mwaikenda.

Alisema pia kutakuwa na maandamano yatakayoanzia Makao Makuu ya Yanga, kabla ya kuanza maandamano hayo wataenda kumtembelea mlezi wao, Mama Fatma Karume na baadae wataelekea Kisiwa Ndui ambapo 'amelala' Mzee Karume kwa ajili ya kufanya dua.

"Msimu huu tumekuja kivingine kabisa, siku ya kilele kuna mambo mengi ya kuwashtukiza wanachama na mashabiki wa Yanga, ikiwamo kutambulisha baadhi ya watu wa benchi la ufundi pamoja na kauli mbiu yetu ya msimu huu"

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Haji Mfikirwa, alisema hii ni shughuli yao wananchi na wanapaswa kujitoa na kamwe hawapaswi kuuangusha uongozi.

Mfikiriwa alisema kila jambo hupimwa mwisho, hivyo siku ya kilele ndio kila kitu kitawekwa hadharani kushuhudia 'suprise matata' tofatuti za zile zilizozoeleka.

Kikosi cha Yanga kiko nchini Morocco wakiendelea kujifua kwa ajili ya kujiimarisha kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara, mashindano ya Kombe la FA na michuano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika

Lakini August 29 Wananchi watapata nafasi ya kuishuhudia timu kwa mara ya kwanza baada ya kuwa imeboreshwa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
3h ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
3h ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE →
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE →
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE →
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →