Nabi aahidi kuunda kikosi cha ubingwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Aug 2021
Nabi aahidi kuunda kikosi cha ubingwa

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amewahakikishia mashabiki wa timu hiyo kuwa msimu ujao ni zamu yao kufurahi

Nabi ameeleza kufurahishwa na usajili uliofanyika kwani umempatia timu yenye sura sahihi ya kupigania mataji

Baada ya kuwashuhudia wachezaji wake katika mazoezi ya kucheza mpira kwa siku mbili, Nabi amepata mwanga wa aina ya timu ambayo itaweza kushindania mataji msimu ujao

"Nimewaangalia wachezaji niliwaambia subirini kwanza nione kwa umakini ubora wa wachezaji ambao wamesajiliwa na sasa niseme msimu ujao tutakuwa na timu imara ambayo itakwenda kupigania heshima ya mataji ya Yanga"

"Niliongea na Ghalib (GSM) kabla ya msimu kumalizika aliniahidi atasajili timu imara na sasa nimeona kweli amekamilisha ahadi yake kwangu na sasa ni kazi yangu na wasaidizi wangu pamoja na wachezaji sasa kuthibitisha ubora wao, hili ni kundi la wachezaji waliokomaa, " Nabi alinukuliwa na Mwanaspoti

Nabi amewataka mashabiki kutokuwa na wasiwasi na timu yao, wasubiri afanye kazi yake, akihitaji takribani siku 90 kutengeneza kikosi cha maangamizi

Nabi amesema ratiba ya wachezaji wake kurudi timu za taifa na muda mfupi kabla ya kuanza mechi za Ligi ya Mabingwa vimeathiri mipango yake

"Tuna kundi la wachezaji wapya ambao ni wengi lakini ukiangalia ligi ilichelewa kumalizika na sasa muda wa maandalizi umekuwa mchache, muda si mrefu kundi kubwa la wachezaji litatawanyika tena na kurudi katika mataifa yao" alisema Nabi

"Wakirudi tutakuwa na siku chache tena kabla ya kuanza mechi za Ligi ya Mabingwa tukianza nyumbani kisha ugenini utaona jinsi mambo yanavyobana lakini niwaambie mashabiki watulie waniachie kazi wasiongeze presha kwa wachezaji, ndani ya siku 90 wataona kitu kikubwa hapa"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
5h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
9h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
10h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
20h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’