Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Injinia Hersi Said, amewahakikishia mashabiki wa Yanga kuwa ujio wa winga Jesus Moloko, utawasahaulisha kuondoka kwa Tuisila Kisinda
Hersi yuko Morocco na kikosi cha Yanga ambacho kinatarajiwa kurejea nchini kukamilisha maandalizi ya mwisho kuelekea kilele cha wiki ya Mwananchi siku ya Jumapili
Hersi amesema Moloko ni mchezaji wa daraja la juu na hana wasiwasi atafanya vizuri katika kikosi cha Yanga
"Jesus Moloko ni mchezaji wa daraja la juu sana, nafikiri ni usajili bora, ukizungumzia mbadala wa Tuisila Kisinda, Moloko ni mzuri zaidi," alisema Hersi
ADVERTISE HERE