Mwishoni mwa wiki hii siku ya Jumapili Wananchi wana jambo lao pale uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo shamrashamra za kuhitimisha wiki ya Mwananchi zitafanyika
Utambulisho wa kikosi cha Yanga, yaani wachezaji na benchi la ufundi kuelekea msimu ujao utafanyika sambamba na utambulisho wa jezi zitakazotumika msiimu ujao
Siku itahitimishwa kwa mchezo wa Kukata na shoka kati ya Yanga dhidi ya Zanaco Fc kutoka Zambia
Uongozi wa Yanga umethibitisha kuwa Zanaco Fc wamealikwa katika hafla hiyo ambayo itaambatana na burudani za kutosha
ADVERTISE HERE