Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Injinia Hersi Said amesema ujio wa aliyekuwa Mkuu wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba, Haji Manara ni mwanzo tu kwani hawashindwi kumchukua mwingine yeyote wanayemuhitaji katika kutimiza malengo ya klabu
Akizungumza baada ya utambulisho wa jezi ya Kimataifa, Hersi alisema malengo ya Yanga kushinda kila taji hivyo hawatashindwa kumchukua yeyote atakayehitajika ili kuhakikisha malengo yanatimizwa
"Sisi tuna malengo makubwa msimu huu, tunataka kushinda kila kombe hivyo niwahakikishie kuwa tutamchukua yeyote tunayemuhitaji, ujio wa Haji (Manara) ni mwanzo tu," alitamba Injinia Hersi
Manara alitambulishwa kutua Yanga jana jioni na moja kwa moja kuanza majukumu yake ya usemaji wa klabu

Manara leo alikuwa muongozaji wa tukio la utambulisho wa jezi mpya za Yanga