Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amewahakikishia Wanachama na Mashabiki kuwa Jumapili katika kilele cha wiki ya Mwananchi watakishuhudia kikosi kamili cha timu hiyo
Aidha Bumbuli amesema msafara wa pili wa wachezaji watatua nchini kesho Ijumaa wakitokea Morocco
Akihojiwa na Wasafi FM mapema leo, Bumbuli alisema baada ya uzinduzi wa jezi bora, mashabiki wajiandae kwa shoo nyingine kubwa Jumapili
Bumbuli amesisitiza kuwa kutokana na ukubwa wa tukio hilo, mashabiki wanapaswa kununua tiketi zao mapema kuepuka kukosa nafasi ya kulishuhudia 'mbashara'
AIdha, amewataka mashabiki wa Yanga wakae tayari kwa sapraizi nyingine siku ya Ijumaa
ADVERTISE HERE