Yanga 'itatisha' msimu ujao - Malima

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Aug 2021
Yanga 'itatisha' msimu ujao - Malima

Beki wa zamani wa Yanga, mkongwe Bakari Malima 'Jembe Ulaya' amesema ana matumaini makubwa kuwa msimu ujao furaha itarejea Jangwani kutokana na usajili makini uliofanywa na GSM

Malima ameeleza kuridhishwa na usajili huo kwani umezingatia mahitaji ya timu kwa wakati huu

Aidha Malima amesema usajili wa wachezaji kutoka DR Congo utainufaisha Yanga kwani wachezaji hao wanafahamiana na hawatahitaji muda mrefu kutengeneza muunganiko

"Msimu ujao Yanga itafanya makubwa sana kwenye Ligi Kuu na Ligi ya Mabigwa Afrika kwa kuwa wachezaji waliosajiliwa wana uzoefu wa michuano ya kimataifa, kamati ya usajili imezingatia kwa kusajili wachezaji wengi kutoka nchi moja (DR Congo), ili kuleta muunganiko wa haraka kutokana na kuelewana hata kwa lugha,” alisema Malima.

Hata hivyo Malima amesema viongozi wa Yanga wanapaswa kumpa muda wa kutosha kocha Nasreddine Nabi ili kuweza kuimarisha kikosi chake kwa kuwa tayari ameonyesha mabadiliko hususan kuimarisha nidhamu ya wachezaji na katika benchi la ufundi.

"Nawaomba viongozi wa Yanga kumpa muda wa kutosha Nabi ili aijenge timu, ameonyesha juhudi kubwa kwa kujenga nidhamu ya wachezaji na hata benchi la ufundi, akipewa muda wa kutosha atafanya makubwa"

Kadhalika, Malima alieleza kufurahishwa na ujio wa aliyekuwa Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, akihamia rasmi Yanga, jambo ambalo alisema atasaidia kufanya makubwa katika klabu hiyo kama alivyokuwa akifanya kwa Wekundu wa Msimbazi hao, endapo akipewa ushirikiano wa kutosha.

Yanga msimu huu itakuwa na wachezaji sita kutoka DR Congo ambao ni Mukoko Tonombe, Heritier Makambo, Yannick Bangala, Fiston Mayele, Shabani Djuma na Jesus Moloko

Mukoko, Djuma, Bangala, Mayele na Moloko wamewahi kucheza pamoja kunako klabu ya AS Vita

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
6h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
10h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
15h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’