Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amewataka Wananchi kuhakikisha wanakamata tiketi zao mapema ili kuwa sehemu ya tukio kubwa kabisa la Wiki ya Mwananchi siku ya Jumapili
Bumbuli amesema muitikio wa mashabiki kununua tiketi ni mkubwa na hivyo kama unataka kushuhudia burudani mbashara pale uwanja wa Benjamin Mkapa, nunua tiketi yako sasa, ukisubiri siku ya tukio unaweza kujilaumu
"Mauzo ya tiketi yameanza kwa muitikio mkubwa. Mpaka kufikia jana tulikuwa tumeuza tiketi zenye thamani ya Million 30. Niwaombe Wananchi wanunua tiketi mapema kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza baadae," alisema Bumbuli


Aidha, wakati shamrashamra kuelekea Siku ya Jumapili zikizidi kushika kasi, Bumbuli amewataka mashabiki wa Yanga wakae tayari kwani siku ya kesho majira ya saa tano asubuhi kutakuwa na jambo kubwa kwa ajili yao