Mpaka ilipofika saa kumi jioni hakukuwa na sehemu ya kukaa kwani uwanja ulikuwa umefurika mashabiki wa Yanga waliojitokeza kwa wingi kushuhudia kilele cha wiki ya Mwananchi
Hakuna mjadala, Yanga ndio klabu yenye mashabiki wengi zaidi Tanzania, hilo limedhihiri leo na litaendelea kudhihiri pale ligi itakapoanza
Kwa wachezaji hasa wageni leo wametambua ukubwa wa timu waliyojiunga nayo na wanapaswa kuipigania timu ili kuwapa raha mashabiki ambao wamejitoa kwa maelfu kuwapokea leo
Haji Manara leo Wananchi wamemduwaza, mapokezi aliyopewa hakuyatarajia
Siku hii kwake itaendelea kubaki katika kumbukumbu katika maisha yake
Nae hakuwaangusha! kwani aliifanya kazi yake kwa ufasaha mkubwa na kuwapa furaha mashabiki waliokuwa wakimshangilia kwa muda wote
Amefanya utambulisho wa wachezaji vile ambavyo wengi walipenda kuona anafanya
Kama ni gari basi limewaka, kazi ni kwa wachezaji kupambana kuhakikisha wanapata matokeo na kuwapa furaha mashabiki




