Zanaco Fc wametupa kipimo kizuri - Nugaz

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Aug 2021
Zanaco Fc wametupa kipimo kizuri - Nugaz

Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amesema mchezo dhidi ya Zanaco Fc umewapa kipimo sahihi katika maandalizi kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Rivers United utakaopigwa Septemba 12 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa

Nugaz amesema lengo la mchezo huo halikuwa kupata matokeo zaidi, bali lilikuwa kuwaonyesha mashabiki timu yao na kocha kuangalia ni wachezaji gani anaweza kuwajumuisha katika kikosi chake cha kwanza

"Sisi matokeo hayatupi shida sana kwani lengo kuu halikuwa matokeo pekee. Shughuli nzima ilikuwa kuwatambulisha wachezaji ili mashabiki wawaone na kocha kuangalia mahitaji ya kikosi chake cha kwanza. Zanaco Fc ni timu nzuri wametupa kipimo sahihi"

"Tumefanya usajili mzuri, wachezaji wameonekana sasa kinachofuata ni jukumu la kocha na benchi lake la ufundi kukiweka sawa kikosi chake. Lakini nikuhakikishie jambo moja, msimu huu ni wetu," alitamba Nugaz

Mchezo huo wa kirafiki uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, ulimalizika kwa Zanaco kupata ushindi wa mabao 2-1

Bao la Yanga lilifungwa na mshambuliaji Heritier Makambo ambaye amerejea na kuendeleza pale alipoishia misimu miwili iliyopita

Pia nyota wengine wapya Jesus Moloko, Yannick Bangala, Shabani Djuma, Dickson Ambundo na Fiston Mayele walipata nafasi katika mchezo huo

Kocha Nasreddine Nabi alifanya mabadiliko ya kikosi chake kwenye kipindi cha pili ikiwa ni pamoja na timu kubadili jezi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’