Feisal Salum 'Fei Toto' anautaka ufalme wake hapa Tanzania, hakika anaweza kuupata msimu huu
Juzi alikuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kilichotambulishwa kwa ajili ya kuwapa furaha Wananchi msimu huu
Bao pekee la Yanga lililowekwa kambani na Heritier Makambo katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Zanaco Fc lilianzia katika mguu wake
Fei Toto aliwapa wakati mgumu Zanaco Fc akitawala eneo la kiungo
Dakika takribani 65 alizocheza kwenye mchezo huo zilitosha kupeleka ujumbe kwa timu pinzani kuwa msimu huu wajiandae 'kisaikolojia'
Fei toto wa sasa anaonyesha ukomavu na kiu ya kufanya mambo makubwa zaidi
ADVERTISE HERE