Mahadhi apania kurudi kikosi cha kwanza Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
6 Jan 2018
Mahadhi apania kurudi kikosi cha kwanza Yanga
Nyota wa Yanga Juma Mahadhi, amesema anataka kuitumia michuano ya Kombe la Mapinduzi kurejesha kiwango chake.

Mahadhi ameanza kwa kasi kwenye kikosi cha Yanga katika michuano hiyo baada ya kuifungia timu hiyo mabao mawili kwenye ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Mlandege.

Mahadhi amekiri kuwa ushindani wa namba ndani ya kikosi cha Yanga umemfanya kutopata muda mwingi kwenye michezo ya ligi kuu.

Alisema kwa sasa anaitumia michuano ya Kombe la Mapinduzi kuinua kiwango chake na kulishawishi benchi la ufundi kumpa nafasi kwenye michezo ya ligi kuu.

“Nashukuru Mungu napata nafasi huku Zanzibar, nataka kuitumia michuano hii kukuza kiwango changu lakini pia kulishawishi benchi la ufundi kunipa nafasi,” alisema Mahadhi.

Aidha, alisema kuwa, kukaa benchi kwenye timu hiyo kunatokana na changamoto ya kuwania namba na hajakata tama ya kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha kocha George Lwandamina.

Yanga tayari imetinga nusu fainali ya michuano ya kombe la Mapinduzi baada ya kushinda michezo yake mitatu ya mwanzo.

Bado ina michezo miwili dhidi ya Zimamoto na Singida United
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE →
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE →
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →