Senzo CEO Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
31 Aug 2021
Senzo CEO Yanga

Uongozi wa klabu ya Yanga umemtangaza aliyekuwa Mshauri wa Mabadiliko Senzo Mazingisa kuwa Mtendaji Mkuu wa klabu (CEO) katika kipindi cha mpito kuelekea mfumo mpya wa Uendeshaji

Akizungumza kwenye Mkutano na Wanahabari mapema leo, Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela alisema Senzo atakuwa Mtendaji Mkuu wa mpito kusimamia yote yaliyopitishwa Katika Mkutano Mkuu wa Wananchama

Aidha Mwakalebela alisema Haji Mfikirwa ambaye alikuwa akikaimu nafasi ya Katibu Mkuu, amerejea katika nafasi yake ya Mkurugenzi wa Fedha na Utawala

Senzo ameushukuru uongozi wa Yanga kwa kumpa nafasi ya kusimamia maazimio yaliyofikiwa kwenye Mkutano Mkuu ili kufikia malengo

Ameahidi kushirikiana na viongozi wengine wa Yanga ili kuhakikisha wanakamilisha mchakato wa Mabadiliko

"Nashukuru sana kwa uongozi wa Yanga kunipa nafasi hii kusaidia kufikia malengo yetu. Sasa ni jukumu langu kuhakikisha Mabadiliko yanakamilika vyema," alisema Senzo

"Nitashirikiana na viongozi wenzangu akiwemo Haji ambaye licha ya kurudi kwenye nafasi yake ya zamani hakuna kitakachobadilika. Tuna kazi moja ya kuhakikisha klabu yetu inafanikiwa"

Nae Mfikirwa aliyekuwa akikaimu nafasi ya Katibu Mkuu, ameushukuru uongozi wa Yanga kwa kumpa nafasi hiyo

"Sasa tunakwenda kuyaishi Mabadiliko, Binafsi nashukuru kwa nafasi niliyokuwa nimepewa kukaimu. Kwa pamoja tutashirikiana kuweza kuifikisha Yanga tunapotaka ifike. Tumkaribishe Senzo kwenye nafasi yake mpya na tumpe ushirikiano wa kutosha"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
19m ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
58m ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
5h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
23h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’