Aliyekuwa mlinda lango wa Yanga Metacha Mnata amesajiliwa na klabu ya Polisi Tanzania kwa mkataba wa miaka miwili
Metacha amejiunga na klabu hiyo baada ya mkataba wake na Yanga kumalizika
Alikuwa kipa namba moja katika kikosi cha Yanga msimu uliopita hata hivyo Yanga ikasitisha uamuzi kumuongezea mkataba baada ya kufanya matukio ya utovu wa nidhamu
Wakati Metacha akitua Polisi Tanzania, Farouk Shikhalo yeye amesajiliwa na klabu ya KMC
Yanga iliachana na makipa huo huku nafasi zao zikichukuliwa na Djigui Diarra kutoka Mali na Erick Johora
ADVERTISE HERE