Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema hakuna kiongozi yeyote wa Yanga aliyekuwa na muda wa kufuatilia jezi za watani zao huku akitaka Yanga isihusishwe na kuvuja kwa jezi za Simba
Mapema leo Kaimu Afisa Habari wa Simba Ezekiel Kamwaga alidai kuna watu wamehujumu jezi zao kwa kuzivujisha mapema kwenye mitandao ya kijamii hivyo kuwalazimu wafanye uzinduzi kabla ya muda waliokuwa wamepanga
Bumbuli amesema Yanga ilishafanya uzinduzi wa jezi bora kabisa hivyo wasihusishwe na kuvuja kwa jezi za Simba kwa kuwa haziwahusu
ADVERTISE HERE