Klabu ya KMC imemtambulisha rasmi mlinda lango Farouk Shikhalo kujiunga na timu hiyo akitokea Yanga
Shikhalo ameondoka Yanga baada ya mkataba wake wa miaka miwili kumalizika huku akiwa sio miongoni mwa wachezaji ambao kocha Nasreddine Nabi alipendekeza waongezwe mikataba
Ukizungumzia mchezaji mwenye nidhamu sana, basi hutakosa kutaja jina la Shikhalo
Kwani katika miaka miwili aliyoitumikia Yanga hakuwahi kusikika akiwa na mgogoro na yeyote pamoja na kuwa zipo nyakati ngumu Yanga ilipitia kabla ya ujio wa GSM
Wakati anajiunga na Yanga akitokea Bandari Fc alikuwa kipa bora, bado anayo nafasi ya kudhihirisha ubora huo katika klabu yake mpya ya KMC

Kila la kheri kipa wa mpira..!
ADVERTISE HERE