Rivers United ni klabu kutoka Port Harcourt, Jimbo la Rivers huko Nigeria. Iliundwa mwaka 2016 baada ya timu za Shark Fc na Dolphins Fc kuungana
Uwanja wao wa nyumbani ni Yakubu Gowon, Uwanja wa zamani wa Ukombozi huko Elekahia ambao unachukua watu 30,000.
Tangu kuundwa kwake mwaka 2016, Rivers United FC imekuwa ikishiriki ligi kuu ya Nigeria
Katika msimu uliopita, Rivers United walishiriki michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF CC) na walifanikiwa kutingia raundi ya kwanza kwa kuiondosha timu ya Afrika Kusini, Bloemfontein Celtic kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-0
Walitolewa katika raundi ya kwanza na ndugu zao Enyimba kwa mikwaju ya penati baada ya matokeo ya jumla ya michezo miwili kuwa 1-1
Msimu huu wamepata tiketi ya kucheza ligi ya mabingwa baada ya kumaliza katika nafasi ya pili ligi kuu ya Nigeria
Ni timu iliyoshiriki michuano ya CAF mara mbili tangu mwaka 2016, msimu huu inashiriki kwa mara ya tatu
Rivers United wamekuwa na matokeo mazuri sana wanapocheza katika uwanja wao wa nyumbani kwani wameshinda mechi zao zote walizocheza nyumbani katika michuano ya CAF
Jumapili ijayo, Septemba 12 wanakutana na Yanga katika hatua ya awali ya michuano ya ligi ya mabingwa
Mchezo wa kwanza unapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam na ule wa marudiano utapigwa huko Nigeria Septemba 19
Yanga inahitaji kupata ushindi mnono katika mchezo wake wa nyumbani ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu raundi ya kwanza
Ni mtihani wa kwanza kwa Kocha Nasreddine Nabi katika michuano ya CAF akiwa na kikosi cha Yanga
Nabi amewahi kutwaa ubingwa wa Shirikisho Barani Afrika mwaka 2013 akiwa na Leopards ya Congo Brazaville
Hivyo ni kocha anayefahamu vyema nini kinahitajika ili kuweza kufanya vizuri katika michuano hii mikubwa zaidi kwa ngazi ya klabu barani Afrika