Wazee Yanga wawakaribisha Senzo, Manara

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Sep 2021
Wazee Yanga wawakaribisha Senzo, Manara

Wazee wa klabu ya Yanga leo wamefanya tukio la kuwakaribisha klabuni Kaimu Mtendaji Mkuu Senzo Mazingisa na Haji Manara ambaye amekabidhiwa kitengo cha Uhamasishaji

Ni kawaida kwa utamaduni wetu Waafrika Wazee wanakuwa na nafasi yao katika klabu, tukio la kuwakaribisha Senzo na Manara ni ishara kuwa wamewapokea kwa mikono miwili na wako tayari kufanya nao kazi

Akizungumza katika tukio hilo lililofanyika Makao Makuu ya klabu ya Yanga Jangwani jijini Dar es salaam, Manara amesema ana deni kubwa kwa Wanayanga kutokana na mapokezi makubwa aliyopata

"Nilipata mapokezi makubwa katika kilele cha wiki ya Mwananchi, nimepokea meseji nyingi za kunikaribisha Yanga, na tukio hili la kukaribishwa klabuni na Wazee ni jambo linalonifanya nijihisi kuwa na deni kubwa kwa Wanayanga"

"Nawaahidi nitawatumikia kwa nguvu zangu zote na nafurahi sasa niko nyumbani. Mimi ni mwenyeji hapa Jangwani, niliwahi kucheza timu ya vijana hapa., achilia mbali wazee wangu kucheza kwa mafanikio makubwa hapa, pia ni Wanachama wa klabu hii" alisema Manara

Aidha kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Rivers United ambao utapigwa Jumapili Septemba 12 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Manara amesema atazungumza na Wanahabari kesho Jumatano kuelezea mikakati ya mchezo huo

"Kesho tutazungumza na Wanahabari kuelekea mchezo wetu dhidi ya Wanaigeria. Lengo letu ni kuona tunashinda kwa idadi kubwa ya mabao ili tuhakikishe mchezo tunaumaliza hapa nyumbani. Tutatangaza kauli mbiu yetu ambayo naamini itatoa hamasa kwa mashabiki wetu na wachezaji kuhakikisha tunafanikisha malengo yetu"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
3h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
22h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’