Mlinda lango Djigui Diarra tayari amerejea katika kikosi cha Yanga kinachojiandaa na maandalizi ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Rivers United ambao utapigwa Jumapili Septemba 12 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amethibitisha kuwa mlinda lango huyo wa Kimataifa wa Mali tayari yuko kambini huku wachezaji wengine watatu wakitarajiwa kurejea kesho
Pamoja na Diarra, wachezaji wengine ambao walikuwa na majukumu ya timu za Taifa ni Khalid Aucho (Uganda), Yannick Bangala ( DRC) na Saido Ntibazonkiza (Burundi)
Wengine ni Feisal Salum, Dickson Job na Bakari Nondo Mwamnyeto ambao walikamilisha majukumu yao katika timu ya Taifa ya Tanzania jana kwa ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Madagascar
ADVERTISE HERE