Taarifa iliyowastua mashabiki wa Yanga leo ni kuhusu ITC za wachezaji watatu Shabani Djuma, Fiston Mayele na Khalid Aucho ambao wanaweza kukosa mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Rivers United utakaopigwa Jumapili, Septemba 12 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema watatolea ufafanuzi kuhusu sintofahamu hiyo katika Mkutano na Wanahabari ambao utafanyika leo
Imeelezwa kuwa Yanga ilipokea ITC za wachezaji hao nje ya muda wa dirisha la usajili wa CAF ambalo lilifungwa August 15
Upo uwezekano kuwa wanaweza kukosa mechi za hatua ya awali na hata raundi ya kwanza kama Yanga itafanikiwa kuvuka

ADVERTISE HERE