Uongozi wa Yanga umetoa ufafanuzi kuhusu kuchelewa kwa ITC za wachezaji watatu Shabani Djuma, Fiston Mayele na Khalid Aucho
Msemaji wa Yanga Haji Manara amesema walichelewa kuzipokea ITC za wachezaji hao licha ya kuwa walikamilisha taratibu za usajili wao kwa wakati
"Tuliwasilisha maombi ya ITC ya Shabani Djuma na Fiston Mayele kwa AS Vita mapema lakini wao wakatuambia tusubiri mpaka August 31, mikataba yao ndio itamalizika. Lakini sisi tuliona muda huo dirisha la usajili CAF litakuwa limefungwa, wametuma ITC nje ya muda hivyo tukaandika barua FIFA kuomba turuhusiwe kuwatumia wachezaji hawa"
"Aucho alikuwa na mgogoro na klabu yake aliyokuwa akiichezea (El Makassa). Alikuwa na madai na klabu hiyo hivyo kuamua kuvunja mkataba na FIFA wakaridhia na kumtangaza yuko huru. Nao wakawa wameweka ngumu kutoa ITC yake kwa wakati. Nae tulishawaandikia barua FIFA kuomba tumtumie"
"Tuna matumaini FIFA watatujibu kabla ya mchezo siku ya Jumapili. Hivyo kwa sasa tusubiri majibu ya FIFA," alisema Manara
Hata hivyo Manara amesisitiza Yanga ina kikosi kipana, akiwatoa wasiwasi mashabiki kuwa hata kama wachezaji hao watakosekana, wapo wengine wa kuchukua nafasi zao
"Yanga imesajili vizuri. Hata wachezaji hawa wakikosekana tunao watu wa kucheza nafasi zao bila ya wasiwasi wowote," aliongeza Manara